YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 8Sample

Soma Biblia Kila Siku 8

DAY 1 OF 31

Msisahau kuwafadhili wageni; maana kwa njia hii wengine wamewakaribisha malaika pasipo kujua (Ebr 13:2). Sisemi kuwa Paulo alikuwa malaika, hapana, ni mwanadamu kama sisi. Ila pia alikuwa ni mtumishi wa Mungu. Kwa hiyo kwa kumfadhili yeye, wenyeji walibarikiwa sana na Mungu, wakaponywa magonjwa yao. Tukio la Paulo kutokupata madhara na nyoka linathibitisha ahadi ya Yesu: Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio ... watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya (Mk 16:17-18).

Scripture

Day 2