YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 8Sample

Soma Biblia Kila Siku 8

DAY 7 OF 31

Waisraeli wanaahidiwa kwamba kuna baraka tele katika kuisikia sauti ya Bwana na kuifuata (m.1-2: Itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo Bwana, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani; na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya Bwana, Mungu wako). Baraka hizi zitajitokeza katika kila kona ya maisha yao, na chemchemi yake ni BWANA. Naye ndiye mwenye kuzishika hizo baraka mkononi mwake, na mwenye mamlaka ya kuzimwaga au kuzizuia. Hivyo wasikengeuke na kwenda kuifuata miungu (m.14). Mpaka leo baraka zote za kiroho zinapatikana kwake Bwana, na hutolewa kwa neema tu kwa yeyote anayemwamini kama Mwokozi wake. Andiko, kwa vile lilivyoona tangu zamani kwamba Mungu atawahesabia haki Mataifa kwa imani, lilimhubiri Ibrahimu habari njema zamani, kusema, Katika wewe Mataifa yote watabarikiwa. Basi hao walio wa imani hubarikiwa pamoja na Ibrahimu aliyekuwa mwenye imani(Gal 3:8-9). Je, umezionja hizo baraka? 

Day 6Day 8

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 8

Soma Biblia Kila Siku 8 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku hasa katika kitabu cha Matendo ya Mitume, Kumbukumbu la Torati, na Yohana pamoja na maelezo yatakayokusaidia kutafakari na kuelewa Neno la Mungu kwa urahisi.

More