YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 8Sample

Soma Biblia Kila Siku 8

DAY 10 OF 31

Maneno ya leo yanatisha sana! Maadui waliotajwa jana wataihusuru miji ya Israeli na kusababisha njaa kali itakayowafanya Waisraeli kula hata watoto wao wanaokufa kwa njaa (m.52-53: Adui atakuhusuru katika malango yako yote kila upande, katika nchi yako yote aliyokupa Bwana, Mungu wako. Nawe utakula uzao wa tumbo lako mwenyewe, nyama ya wana wako na binti zako aliokupa Bwana, Mungu wako). Hizo laana zote zitakuja kwa kuwa hukuisikiza sauti ya BWANA, kushika maagizo yake na amri zake alizokuagiza(m.45). Hiyvo watu wataacha kumtumikia Bwana kwa furaha na moyo wa kushukuru (m.47). Lakini kujitengulia utawala wa Bwana italeta utawala mwingine ambao utawalemea sana. Zingatia m.48: Utawatumikia adui zako atakaowaleta Bwana juu yako, kwa njaa, na kwa kiu, na kwa uchi, na kwa uhitaji wa vitu vyote; naye atakuvika kongwa la chuma shingoni mwako, hata atakapokwisha kukuangamiza. Ndugu, ubaki kwa Bwana!

Day 9Day 11