YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 8Sample

Soma Biblia Kila Siku 8

DAY 2 OF 31

Paulo alipowaona alimshukuru Mungu, akachangamka(m.15). Ndugu Wakristo wa Rumi walikuja kumlaki Paulo, akafurahi sana. Miaka ya nyuma aliwaandikia barua (Waraka kwa Warumi), na mara kwa mara alipata habari zao kwa njia ya ndugu waliosafiri kutoka huko. Kwa muda mrefu alikuwa na mpango wa kufika kwao, kwa sababu alikuwa na hamu sana ya kuwaona. Ndiposa akafika. Mungu mwenyewe alimfikisha! Angalia kwamba hata hapa Paulo alifuata utaratibu wake wa kila mahali kwamba Injili ni kwa Myahudi kwanza(Rum 1:16). Kwa hiyo hata siku ya tatu baada ya kufika Rumi, alikutana na wakuu wa Wayahudi.

Scripture

Day 1Day 3