Soma Biblia Kila Siku 6Sample
Sasa uenezaji wa Injili ulipiga tena hatua muhimu mbele. Atheneni mji mkuu wa Ugriki. Ulikuwa ni kitovu cha falsafa na mahojiano kuhusu dini. Rudia m.19-22:Waathene na wageni waliokaa huko walikuwa hawana nafasi kwa neno lo lote ila kutoa habari na kusikiliza habari za jambo jipya.Paulo akasimama katikati ya Areopago, akasema, Enyi watu wa Athene, katika mambo yote naona ya kuwa ninyi ni watu wa kutafakari sana mambo ya dini. Kabla Warumi hawajawa watawala kuna kipindi ambacho watawala wa dunia walikuwa ni Wagriki. Kwa kipindi hicho lugha yao ilienea sana. Kila mahali alipofika Paulo aliweza kutumia lugha ya Kigriki kama ilivyo kwa Kiingereza siku hizi. Pamoja na lugha yao pia imani yao ilienea sana. Waliamini na kuabudu mchanganyiko wa miungu mingi. Zingatia wito wa m.30-31: Zamani zile za ujinga Mungu alijifanya kama hazioni; bali sasa anawaagiza watu wote wa kila mahali watubu. Kwa maana ameweka siku atakayowahukumu walimwengu kwa haki, kwa mtu yule aliyemchagua; naye amewapa watu wote uthabiti wa mambo haya kwa kumfufua katika wafu.
Scripture
About this Plan
Soma Biblia Kila Siku 6 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kutafakari na kuelewa Neno la Mungu kwa urahisi.
More