YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 6Sample

Soma Biblia Kila Siku 6

DAY 30 OF 30

Tafakari maneno haya pamoja na Sefania 2:3, Mtafuteni Bwana, enyi nyote mlio wanyenyekevu wa dunia, ninyi mliozitenda hukumu zake; itafuteni haki, utafuteni unyenyekevu; huenda mtafichwa katika siku ya hasira ya Bwana. Tunaitwa kumtafuta Mungu kila siku ya maisha yetu kwa kutega sikio letu kusikia neno lake ili atushikie hatua za mienendo yetu. Tukiweka bidii katika jambo hili, Mungu atatufinyanga upya tupate kipawa cha kumcha na kutushikamanisha naye. Ufahamu ulio bora ni ule unaomwelekea Mungu. Kwa hiyo wito wa leo ni kuweka bidii katika kumtafuta Mungu. Fanya hivyo kwa kuomba na kujifunza Neno lake kwa bidii. Hivyo utaongezeka maarifa ya kumwishi Mungu!

Day 29