Soma Biblia Kila Siku 6Sample
Kitabu cha Danieli kinagawanyika katika sehemu mbili: Dan 1-6 ni historia, wakati Dan 7-12 zinahusu maono na hali ijayo. Sasa sio watawala tena wanaoota ndoto na kutafsiriwa na Danieli, bali mwenyewe ndiye apataye maono. Njozi hii inalandana na Ufu 12:3-5: Ikaonekana ishara nyingine mbinguni; na tazama, joka kubwa jekundu, alikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na juu ya vichwa vyake vilemba saba. Na mkia wake wakokota theluthi ya nyota za mbinguni, na kuziangusha katika nchi. Na yule joka akasimama mbele ya yule mwanamke aliye tayari kuzaa, ili azaapo, amle mtoto wake. Naye akazaa mtoto mwanamume, yeye atakayewachunga mataifa yote kwa fimbo ya chuma. Na mtoto wake akanyakuliwa hata kwa Mungu, na kwa kiti chake cha enzi. Licha ya wanyama hawa kutisha, lakini kutisha kwao hakudumu. Falme za dunia na wapinzani wa Mungu hawadumu. Simba na chui watachinjwa. Historia ya mwanadamu inabaki mikononi mwa Mungu tu (ling. m.11-12 na Ufu 19:20, Nikatazama wakati huo; kwa sababu ya sauti ya yale maneno makubwa iliyoyasema ile pembe; nalitazama hata mnyama yule akauawa, mwili wake ukaharibiwa, akatolewa ateketezwe kwa moto. Na kwa habari za wale wanyama wengine, walinyang'anywa mamlaka yao; walakini maisha yao yalidumishwa kwa wakati na majira.↔ Yule mnyama akakamatwa, na yule nabii wa uongo pamoja naye, yeye aliyezifanya hizo ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile chapa ya huyo mnyama, nao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa wangali hai katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti).
Scripture
About this Plan
Soma Biblia Kila Siku 6 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kutafakari na kuelewa Neno la Mungu kwa urahisi.
More