YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 6Sample

Soma Biblia Kila Siku 6

DAY 29 OF 30

Maono ya Danieli yana ujumbe unaokuja kwa njia ya picha za wanyama. Kondoo dume ni mfano wa ufalme wa Umedi-Uajemi (pembe kubwa ikiwa Umedi), wakati mbuzi ni Ugriki (8:21, Yule beberu, mwenye manyoya mengi, ni mfalme wa Uyunani). Alivyoona Danieli, Ugriki uligawanyika katika tawala nne. Hapo alitokea Antiokio Epifani kutawala nchi ya Uzuri (= Israeli; m.9) akinajisi hekalu la Yerusalemu (akifafanishwa na pembe ndogo, imeandikwa juu yake katika m.11:Ikajitukuza hata juu yake aliye mkuu wa jeshi hilo, ikamwondolea sadaka ya kuteketezwa ya daima, na mahali pa patakatifu pake pakaangushwa chini). Huyu ni mfano wa mpinga Kristo atakayekuja. Angalia kuwa kutawala kwake kuna ukomo. Mungu mwenye mamlaka ya kimbingu ameshamwekea muda. Ni faraja letu.

Scripture

Day 28Day 30