YouVersion Logo
Search Icon

Plan Info

Soma Biblia Kila Siku 6Sample

Soma Biblia Kila Siku 6

DAY 1 OF 30

Ilikuwa lazima neno la Mungu linenwe kwenu kwanza; lakini kwa kuwa mnalisukumia mbali ... angalieni, twawageukia Mataifa (m.46). Ni nini kilichowafanya Wayahudi wasiipokee Injili? Ni wivu : Watu wengi, karibu mji wote, wakakusanyika walisikie neno la Mungu. Bali Wayahudi, walipowaona makutano, wakajaa wivu, wakayakanusha maneno yaliyonenwa na Paulo, wakibisha na kutukana (m.44-45)! Ole wao! Je, mtumishi wa Kanisa la Bwana, unamwonea mtumishi mwenzako wivu akipata ufunuo ambao wewe hukupata? Acha wivu wako. Sikiliza ujumbe wake; usije ukakosa uzima wa milele! Wayahudi walikuwa wa kwanza! Ndivyo waumini kanisani tulivyo wa kwanza leo kuupokea uamsho wa Injili! Tusiipoteza nafasi yetu!

Scripture

Day 2

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy