YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 6Sample

Soma Biblia Kila Siku 6

DAY 6 OF 30

Luka aliyeandika Injili pia ni mwandishi wa kitabu hiki. Kwa kitabu hiki alitaka kuonyesha jinsi agizo la Yesu la Matendo 1:8 lilivyotekelezwa: Mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi. Alitaka kueleza jinsi Injili ilivyoenea na kushinda hatua kwa hatua kuanzia Yerusalemu hadi mji mkuu wa ulimwengu wa wakati ule, mji wa Rumi. Kwa safari ya Paulo ya kwanza ya misioni Injili ilipata kuenea Asia (leo panaitwa Uturuki). Kabla hajaondoka kwenda safari ya pili ulifanyika mkutano wa mitume katika usharika mama Yerusalemu. Hapo walihitaji wafanye uamuzi katika suala muhimu.

Scripture

Day 5Day 7