YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 6Sample

Soma Biblia Kila Siku 6

DAY 11 OF 30

Leo tubarikiwe na maneno mawili. 1.Basi alipokwisha kuyaona yale maono, mara tukataka kutoka kwenda Makedonia, kwa kuwa tuliona hakika ya kwamba Mungu ametuita tuwahubiri Habari Njema(m.10). Hapa tunaelezwa jinsi Injili ilivyofika Ulaya kwa mara ya kwanza maana Makedonia ni sehemu ya Ulaya. Katika hili waliongozwa na Roho Mtakatifu: Wakapita katika nchi ya Frigia na Galatia, wakikatazwa na Roho Mtakatifu, wasilihubiri lile neno katika Asia. Walipofika kukabili Misia wakajaribu kuenda Bithinia, lakini Roho wa Yesu hakuwapa ruhusa(m.6-7)! Mungu mwenyewe aliyataka haya. Alifungua mlango mpya. 2.Moyo wake Lidia ulifunguliwa na Bwana: Akatusikiliza, ambaye moyo wake ulifunguliwa na Bwana, ayatunze maneno yaliyonenwa na Paulo (m.14). Ni kwa nguvu ya Bwana tu twaweza kufunuliwa Injili na kuokoka!

Scripture

Day 10Day 12

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 6

Soma Biblia Kila Siku 6 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kutafakari na kuelewa Neno la Mungu kwa urahisi.

More