YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 6Sample

Soma Biblia Kila Siku 6

DAY 4 OF 30

Wakawazuia makutano kwa shida, wasiwatolee dhabihu (m.18). Paulo na Barnaba walihubiri Injili Listra (m.7). Mtu aliyekuwa kiwete tangu tumboni mwa mamaye akawasikiliza kwa imani. Mara Paulo akamponya akaanza kutembea (m.8-10). Mwujiza kama huu walikuwa hawajawahi kuona Listra, wakafikiri miungu yao, Zeu na Herme imewashukia. Wakataka kuwatolea dhabihu (m.11-13). Lakini wakawazuia wakisema: Sisi nasi tu wanadamu hali moja na ninyi; twawahubiri habari njema, ili mgeuke (m.15)! Je, wewe umegeuka? 

Scripture

Day 3Day 5