YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 6Sample

Soma Biblia Kila Siku 6

DAY 19 OF 30

Suala la ubatizo limezungumzwa sana Tanzania. Ni muhimu tusijenge mafundisho ya ubatizo juu ya somo moja tu. Ni lazima tujenge juu ya mafundisho yote ya Agano Jipya ili tuwe na imani safi (Efe 2:20,Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni)! Ukitaka kufuata maneno yale tu yanayopatana na hoja zako hujawa mtii kwa Roho Mtakatifu. Maana yeye aliwaongoza Mitume katika yote waliyoandika (2 Pet 1:20-21, Hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu). Ni kama vile Yesu alivyowaahidi (Yn 14:26,Huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia; Yn 16:13,Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote). Fundisho la leo: Kumpokea Roho Mtakatifu kunakwenda sambamba na ubatizo, yaani, ubatizo wa kikristo: Wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu. Na Paulo, alipokwisha kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao(m.5-6).

Scripture

Day 18Day 20