YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 6Sample

Soma Biblia Kila Siku 6

DAY 21 OF 30

Neno la Bwana lilizidi kushinda kwa nguvu kwa watu Waefeso na Asia yote (m.20). Ndipo akajitokeza huyu bwana Demetrio. Aliogopa kupoteza biashara yake nzuri na utajiri wake. Kazi ya Paulo iliharibu biashara yake maana watu wengi walianza kumwabudu Yesu Kristo badala ya Artemi. Akafanya mbinu. Akaanza kudai kuwa Paulo huondoa utukufu wa Artemi na hivyo huondoa utukufu wa Efeso. Ndipo ghasia ikatokea. Ila Paulo hakuwa mkorofi, bali alijulikana kama mtu mwema mwenye heshima: Baadhi ya wakuu wa Asia, walio rafiki zake [Paulo], wakatuma watu kwake, wakimsihi asijihudhurishe nafsi yake ndani ya mahali pa michezo(m.31).Mmewaleta watu hawa, wasioiba vitu vya hekalu wala kumtukana mungu mke wetu(m.37). Na katika Warumi 12:17 Paulo aliandika: Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote.Kama yamkini, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote. Na sisi, je?

Scripture

Day 20Day 22