BibleProject | Hekima ya MithaliPrøve

BibleProject | Hekima ya Mithali

Dag 1 av 32

Kitabu cha Mithali ni sehemu ya vitabu vya hekima vya Biblia. Vitabu vya hekima vya Biblia huangazia swali, "Je, inamaanisha nini kuishi vyema katika ulimwengu wa Mungu?" Hebu ichukulie kuwa "Maisha Mema, kwa binadamu."

Vitabu vya hekima ni vya aina mbalimbali: nyimbo, simulizi, fikira na mapenzi. Kitabu hiki kimsingi ni aina moja ya uandishi uitwao mithali. Mithali ni kauli fupi, yenye maana nzito na iliyojaa hekima. Mithali ni aina ya ushairi. Hata hivyo, muundo wa ushairi wa Kiebrania ni tofauti na mashairi ya Kiswahili.

Ushairi wa siku za leo (fikiria kuhusu kadi za salamu) kwa kawaida hufanya mistari miwili kuwa na vina kwenye maneno yake ya mwisho. Ushairi wa kiebrania, kwa upande mwingine, una mistari miwili ambayo haina vina ila inalingana kimaudhui. Mstari wa pili katika shairi la Kiebrania unashindilia maana ya mstari wa kwanza, lakini kwa kutumia maneno tofauti. Kitabu hiki kimejaa mkusanyiko wa kauli hizi fupi za kishairi zenye hekima ziitwazo mithali.

Kitabu cha Mithali huangazia jinsi ya kuishi maisha bora iwezekanavyo kwenye dunia ya Mungu. Mithali zenyewe ni fupi fupi, lakini zimejaa busara! Mithali huangazia mambo muhimu ya kujifunza maishani na hushughulikia kikamilifu utata wa maisha.

Sulemani ndiye aliandika mithali nyingi zaidi—lakini sio zote. Kitabu chenyewe kinaonekana kuwa kazi ya mtu aliyekuja baadaye ambaye alikitayarisha jinsi kilivyo. Sulemani aliandika angalau mithali 3,000, lakini ni chache tu kati ya hizo zilijumuishwa katika kitabu hiki.

Tunapochambua kitabu hiki cha kale cha hekima, tutaangazia kwa makini maneno na maudhui muhimu yatakayotuelekeza kwenye ujumbe mkuu unaoangaziwa hapa. Tutaona kuwa maudhui kama vile "Kumcha Mungu"
yameangaziwa kwenye kitabu kizima.

Tunapoanza, utagundua kuwa sura za kwanza tisa sio mithali, lakini ni mifululizo ya mashairi yanayokuchochea na kukupa sababu ya kusoma mithali. Mashairi haya yanasimulia hekima ya Mungu na umuhimu wake maishani mwetu.

Hebu tuanze! Ikiwa hujatazama video yetu ya muhtasari wa kitabu cha Mithali, tunapendekeza ufanye hivyo kwanza kabla ya kuanza sura ya 1.

Dag 2

Om denne planen

BibleProject | Hekima ya Mithali

Kitabu cha Mithali kinasema kuwa hekima ya Mungu imedhihirishwa kupitia ulimwengu na unaalikwa kushiriki. Je, ni lipi chaguo la busara kuhusiana na pesa, kazi, uhusiano na shughuli za kimaisha za kila siku? Mwongozo huu wa siku 32 utakuwezesha kusoma kitabu cha Mithali hatua kwa hatua na kufahamu mwelekeo unaopaswa kuchukua.

More