BibleProject | Hekima ya MithaliPrøve
Sura ya 5: Kukataa Mwanamke Mpumbavu
Baba Anazungumzia na Mwanawe Mara ya Nane
Kuna mhusika katika Mithali, mwanamke mzinzi, ambaye hadi sasa tumekumbana naye kwa kifupi (2:16-19). Sasa katika sura ya 5-7, tunafahamu zaidi kuhusu mwanamke huyu na haipendezi. Mwanamke huyu ni mnafiki na hatakufanyia mazuri.
Kauli hii inatisha. Baba anamwita mwanamke mzinzi "mwanamke usiyestahili kuwa na uhusiano naye." Kauli, "usiyestahili kuwa na uhusiano naye", inaashiria mwanamke huyu ameolewa. Jihadhari! Huenda akawa mshawishi, mwenye kinywa "kinachodondoka asali" na maneno yaliyo "laini kuliko mafuta," lakini kwa kweli yeye ni mwenye makali na uchungu. Ukimfuata mtaelekea naye "moja kwa moja hadi kaburini."
Baba anaendelea na kutumia taswira linganifu: nyumba ya mwanamke mzinzi ni chanzo cha uharibifu, lakini nyumbani kwa mkeo ni tunda la maisha. Baba anamlinganisha mke na maji ("kisima" na "chemchemi"). Katika eneo la Asia ya Magharibi, maji yalikuwa yanakata kiu kutokana na hali ya joto kali. Vivyo hivyo, baba anaashiria, mke ni maji kwa roho ya mme wake. Mwanamme mwenye kiu cha mapenzi anapaswa kutoshelezwa na mkewe na kulewa kwenye mahaba yake, na kamwe asishughulike na mwanamke mwingine.
Baba anamwambia mwanawe "furahia katika mke wa ujana wako" (18). Huu ni wito wa kufurahia uhusiano wa kimapenzi na mwenzi wako wa ndoa. Kunywa maji safi ya ndoa na usiguse maji yaliyochafuliwa ya mwanamke mzinzi. Ikiwa una mke au mme, shukuru kwa ajili ya mwenzi wako unaposoma sura hii, na ujiulize jinsi mnavyoweza kufurahia zaidi upendo wenu. Ikiwa hujaingia katika ndoa, mwombe Mungu akupe uvumilivu usubirie maji safi.
Skriften
Om denne planen
Kitabu cha Mithali kinasema kuwa hekima ya Mungu imedhihirishwa kupitia ulimwengu na unaalikwa kushiriki. Je, ni lipi chaguo la busara kuhusiana na pesa, kazi, uhusiano na shughuli za kimaisha za kila siku? Mwongozo huu wa siku 32 utakuwezesha kusoma kitabu cha Mithali hatua kwa hatua na kufahamu mwelekeo unaopaswa kuchukua.
More