BibleProject | Hekima ya MithaliPrøve

BibleProject | Hekima ya Mithali

Dag 11 av 32

Sura ya 10: Maneno na Utajiri

Sura hii ni mwanzo wa mithali zenyewe. Hii ni misemo mifupi ya mistari miwili ambayo ni rahisi kukumbuka na kutumia.

Mithali hizi zinaanzia 10.1 hadi 22:16 na tunaelezwa kwamba ziliandikwa na Mfalme Sulemani. Tunafahamu kuwa zimepangwa kwa utaratibu na angalau kwa jumla: kuna mithali 375 katika sehemu hii, na cha kusisimua, neno "Sulemani" (שְׁלֹמֹ) katika Kiebrania linafikia ujumla wa nambari 375! Misemo hii imeandaliwa kwa ajili yetu ili tusome na tutafakari.

Kati ya mithali zote katika sura ya 10, maudhui mawili yanaangaziwa: maneno na utajiri.

Kuna msisitizo kuhusu uwezo wa maneno yetu na jinsi yanavyoweza kusababisha mazuri au kuleta maafa. "Mpumbavu anayepayuka" hadhibiti kinywa chake (8, 10) na huleta uharibifu (14). Kinyume chake "Kinywa cha mwenye haki ni chemchemi ya uhai," na huongeza thamani kwa wengine (11, 16, 20).

Pia utagundua kwamba mstari wa 2-5 inazungumzia utele au umaskini kama matokeo ya muda mrefu ya tabia za mtu. "Mikono mivivu husababisha umaskini," lakini Mungu hupenda kubariki "mikono yenye bidii" na kazi ya bidii ya wenye busara (22).

Unaposoma mithali mbalimbali, zingatia jinsi utajiri unavyopatikana au kupotea. Wakati mwingine uamuzi wetu huchangia pakubwa, lakini pia hali tusizoweza kuepuka huchangia mara kwa mara. Je, hili linakusaidia vipi kumcha Mungu hasa kupitia pesa na mali yako?

Dag 10Dag 12

Om denne planen

BibleProject | Hekima ya Mithali

Kitabu cha Mithali kinasema kuwa hekima ya Mungu imedhihirishwa kupitia ulimwengu na unaalikwa kushiriki. Je, ni lipi chaguo la busara kuhusiana na pesa, kazi, uhusiano na shughuli za kimaisha za kila siku? Mwongozo huu wa siku 32 utakuwezesha kusoma kitabu cha Mithali hatua kwa hatua na kufahamu mwelekeo unaopaswa kuchukua.

More