BibleProject | Hekima ya MithaliPrøve

BibleProject | Hekima ya Mithali

Dag 14 av 32

Sura ya 13: Njia Mbili, Njia Moja

Mstari wa 1 unaendeleza yaliyomo katika sura 9 za kwanza— mwana mwenye busara kusikiliza ushauri wa babake. Maadili ya kuwa mwenye kufunzika yamerudiwa mara nyingi katika sura hii (tazama mstari wa 1, 10 na 18). Mwana mwenye busara hupokea ushauri, lakini mpumbavu "hakubali kukosolewa" na hujiangamiza mwenyewe.

Kumbuka, kulingana na Mithali kuna aina mbili tu za watu: mwenye haki, mtu mwenye busara na mpumbavu mwovu. Kulingana na sura hii, utajua tofauti kwa maneno wanayotamka, vitu wanavyopenda, mienendo yao, na hata, kishairi, kwa harufu yao! ("Waovu hujitengenezea uvundo wenyewe..." Ni mtazamo wa wazi kabisa wa maisha, na kusudi lake ni kukushawishi kwamba kuna njia moja tu ya kuishi katika kweli na haki.

Kuongezea, tazama kwa makini mstari wa 12 na 19, yote miwili inahusu "kutimizwa kwa haja" zako. Kutimizwa kwa haja kumefafanuliwa kama mti wa uzima, utamu kwa moyo na "urithi kwa watoto wa watoto [wako]." Maisha haya ni kwa wenye haki pekee.

Unaposoma sura hii, angalia jinsi imegawanywa kwenye mstari wa 1, 10 na 18. Jiulize ikiwa hivi karibuni umekuwa unafundishika. Je, unawezaje kutembea katika njia ya haki?

Dag 13Dag 15

Om denne planen

BibleProject | Hekima ya Mithali

Kitabu cha Mithali kinasema kuwa hekima ya Mungu imedhihirishwa kupitia ulimwengu na unaalikwa kushiriki. Je, ni lipi chaguo la busara kuhusiana na pesa, kazi, uhusiano na shughuli za kimaisha za kila siku? Mwongozo huu wa siku 32 utakuwezesha kusoma kitabu cha Mithali hatua kwa hatua na kufahamu mwelekeo unaopaswa kuchukua.

More