BibleProject | Hekima ya MithaliPrøve
Sura ya 18: Zungumza Machache, Sikiliza Zaidi
Sura hii inazungumzia mada tofauti, lakini maudhui mawili yaliyojirudia ni kusikiliza na kuzungumza. Inaonekaka kuwa mambo haya mawili yanahusiana.
Angalia maneno yanayoashiria kusikiliza kama vile "tafuta," "sikia," "elewa," "pata," na "chunguza." Umetambua chochote? (Dokezo: kadri unavyosikiliza zaidi, ndivyo unazidi kuwa mwenye hekima.) Sasa angalia maneno yanayoashiria kuzungumza kama vile "midomo," kinywa," na "ulimi." Tunatambua sifa kuu ya mpumbavu— mtu asiyependa kusikiliza, lakini anapenda kuzungumza.
Hata hivyo, sio vibaya kuzungumza! Tazama mstari wa 20 hadi 21. Mtu mwerevu sio mwepesi wa kuzungumza; maneno yake hujenga. Kuna sitiari nzuri pale: tunda la kinywa cha mtu huridhisha. Tunda haliwezi kuzalishwa kwa haraka, lakini hukua baada ya muda na utunzaji pia. Maneno yetu yanaweza kuwa na manufaa sana, ikiwa tu tutajifunza kusikiliza (tazama mstari wa 13).
Unapopitia misemo hii ya hekima, tafakari kuhusu jinsi unavyoweza kuimarisha uhusiano maishani kwa kusikiliza na kuzungumza kwa uangalifu.
Skriften
Om denne planen
Kitabu cha Mithali kinasema kuwa hekima ya Mungu imedhihirishwa kupitia ulimwengu na unaalikwa kushiriki. Je, ni lipi chaguo la busara kuhusiana na pesa, kazi, uhusiano na shughuli za kimaisha za kila siku? Mwongozo huu wa siku 32 utakuwezesha kusoma kitabu cha Mithali hatua kwa hatua na kufahamu mwelekeo unaopaswa kuchukua.
More