BibleProject | Hekima ya MithaliPrøve
Sura ya 22: Misemo ya Wenye Busara
Sura hii inaweza kugawanywa katika sehemu mbili. Mithali 375 alizoandika Sulemani zinakamilika katika sehemu ya kwanza ya sura hii (mstari wa 1-16) Hizi za mwisho 16 zinazungumzia ufanisi na zinahimiza wenye mali nyingi waishi kulingana na kanuni za Mungu za utajiri. Mali aipendayo zaidi Mungu ni haki! Ukweli huu unadhihirishwa kupitia kifungu cha 8-9, katika mistari hii 16, ambapo inazungumzia kuhusu ukarimu kwa maskini.
Mstari wa 17-21 ni utangulizi wa sehemu mpya katika kitabu cha Mithali iitwayo "Misemo Thelathini ya Wenye Busara" (kutoka 22:17-24:22). Kundi hili lina misemo thelathini. Ya kwanza sita inapatikana katika sura hii. Misemo hii ni tofauti na mithali za mistari miwili ambazo tumezoea kusoma. Misemo hii kwa kawaida ni mirefu zaidi (mistari 4-6), ingawa baadhi yake ni ya mstari mmoja mmoja(tazama 22:28).
Kabla ya kuanza msemo, tusome utangulizi (mstari wa 17-21) unaotukumbusha maneno ya baba. Ikiwa hukumbuki, ni yule anayemzungumzia mwanawe katika sura ya 1-9. Anamsihi mwana kusikiliza hekima na kutumia maarifa, au, kama anavyosema katika mstari wa 19, "Imani yako iwe kwa Yahweh." Kumtumaini Mungu ndilo kusudi la kitabu hiki cha kale cha hekima. Soma tena mstari wa 17-21, na utafakari kuhusu kusudi la moyo wa baba kwako.
Skriften
Om denne planen
Kitabu cha Mithali kinasema kuwa hekima ya Mungu imedhihirishwa kupitia ulimwengu na unaalikwa kushiriki. Je, ni lipi chaguo la busara kuhusiana na pesa, kazi, uhusiano na shughuli za kimaisha za kila siku? Mwongozo huu wa siku 32 utakuwezesha kusoma kitabu cha Mithali hatua kwa hatua na kufahamu mwelekeo unaopaswa kuchukua.
More