BibleProject | Hekima ya MithaliPrøve
Sura ya 25: Hekima Mbele ya Wakubwa Wako
Sura ya 25 ndio mwanzo wa sehemu kuu ya tano ya Mithali. Hebu tupitie tulichojifunza hadi sasa:
•Sehemu ya 1 (sura ya 1-9) inahusu hotuba ya baba kwa mwanawe.
•Sehemu ya 2 (sura ya 10-22:16) inahusu misemo 375 ya Sulemani.
•Sehemu ya 3 (sura ya 22:17-24:22) inaanza “Misemo Thelathini ya wenye Busara.”
•Sehemu ya 4 (sura ya 24:23b-34) inaendeleza “Misemo ya Ziada ya Wenye Busara.”
•Sehemu ya 5 (sura ya 25-29) inaendeleza mithali zaidi za Sulemani.
Tunafahamu kutoka kwa 1 Wafalme 4:32 kuwa Sulemani alikuwa mwenye hekima nyingi na aliandika maelfu ya mithali, japo kuna watu wengine walihusika katika kupanga na kuhariri kitabu hiki. Dokezo la kuvutia ni kuwa sehemu ya 5 ilikusanywa na Mfalme Hezekia miaka 250 baada ya Sulemani (25:1).
Sehemu hii ya Mithali inahusu kuwakuza viongozi. Sura ya 25-27 inahusu wanaowahudumia wafalme, nayo sura ya 28-29 inawazungumzia walio kwenye nyadhifa za mamlaka. Hebu chukulia unamtumikia mfalme—utahitaji kujua tabia sahihi za kifalme, utaratibu, na unachopaswa kufanya. Pia utahitaji kujifunza jinsi ya kutatua migogoro, kuzima moto hasa katika hali iliyojaa wasiwasi, au kujitetea.
Maarifa hayo yote yako hapa! Sura ya 25 ni mwongozo kuhusu unachostahili kufanya ukiwa katika mazingira ya hadhi ya juu. Ikiwa wewe ni balozi wa nchi au msemaji wa kampuni, wakala wa mteja au mpatanishi wa marafiki na familia, utajifunza mengi hapa. Je, ni nini ambacho huenda Bwana akakufundisha leo kuhusu namna ya kuendeleza shughuli zako muhimu?
Skriften
Om denne planen
Kitabu cha Mithali kinasema kuwa hekima ya Mungu imedhihirishwa kupitia ulimwengu na unaalikwa kushiriki. Je, ni lipi chaguo la busara kuhusiana na pesa, kazi, uhusiano na shughuli za kimaisha za kila siku? Mwongozo huu wa siku 32 utakuwezesha kusoma kitabu cha Mithali hatua kwa hatua na kufahamu mwelekeo unaopaswa kuchukua.
More