BibleProject | Hekima ya MithaliPrøve

BibleProject | Hekima ya Mithali

Dag 20 av 32

Sura ya 19: Nyumba ya Wapumbavu

Kusoma sura hii yote ni kama kutembelea nyumba ya wapumbavu. Sogea karibu! Katika onyesho utaona "shahidi wa uongo," "mwana mpumbavu,"asiye na kazi," mtu mwenye hasira kali," mtu mvivu," "mkatili," na "mtu asiyeheshimika." Kila mpumbavu ana ishara inayoonyesha hatima yake, na kiukweli ni mwisho usio mwema. Usiharakishe kusoma hapa, pitia taratibu. Chukua muda wako na utazame kwa makini. Tahadhari kwa msomaji: usiwe kama watu hawa!

Mingi ya misemo hii inakuonya kuhusu uovu. Hata hivyo, sura hii imejaa misemo kuhusu watu ambao wameonyesha uadilifu, uamuzi mzuri, ukarimu, maagizo, uaminifu na kumcha Mungu. Linganisha hatima yao na watu waovu. Ungependa hatima yako iwe vipi?

Pia, angalia jinsi Mungu Anavyowachukulia maskini na wenye ufukara katika mstari wa 1, 4, 7, 17 na 22. Maskini husahaulika na kudhulumiwa mara nyingi, lakini Mungu hawaachi. Kwa kweli, Mungu anawapenda maskini wanaoishi katika njia ya haki na huwainua juu ya wapumbavu.

Je, ni mpumbavu yupi kati ya hawa anatumika kukuonya zaidi? Je, nini unachopaswa kujifunza ili kuepuka hatima yao?

Dag 19Dag 21

Om denne planen

BibleProject | Hekima ya Mithali

Kitabu cha Mithali kinasema kuwa hekima ya Mungu imedhihirishwa kupitia ulimwengu na unaalikwa kushiriki. Je, ni lipi chaguo la busara kuhusiana na pesa, kazi, uhusiano na shughuli za kimaisha za kila siku? Mwongozo huu wa siku 32 utakuwezesha kusoma kitabu cha Mithali hatua kwa hatua na kufahamu mwelekeo unaopaswa kuchukua.

More