BibleProject | Hekima ya MithaliPrøve

BibleProject | Hekima ya Mithali

Dag 17 av 32

Sura ya 16: Kuwa mwenye Busara Mbele ya Mungu

Sura ya 10-15 ina mithali zinazotumia utofautishaji kufundisha. Sura ya 16 inatumia mtindo mpya wa ulinganishaji. Kimsingi, neno "lakini, lakini, lakini" katika sura ya 12 halitumiki na badala yake "na, na, na" inatumika. Misemo hii linganifu hutaja wazo moja kuu kisha inalichambua kwa njia mbili. Ni kama kuangalia kitu ukitumia jicho moja kisha ukitazame tena kwa macho yote. Utaona kina na umuhimu wake kwa njia mpya.

Sura hii inaendelea kutumia jina la agano la kinibafsi la Mungu, Yahweh. Kati ya mithali 375 za Sulemani (10:1-22:16) ni 55 tu zinatumia jina Yahweh na karibu nusu ya hizi zinapatikana katika sura hizi mbili (mara 9 katika sura ya 15, mara 11 katika sura ya 16). Je, unadhani kwa nini jina la Mungu limetumika mara nyingi hivi?

Mithali hizi zimegawanywa katika sehemu kuu tatu: Hekima ya kuishi mbele ya Yahweh (mstari wa 1-9), hekima kuhusu kusimama mbele za mfalme (mstari wa 10-15), na hekima ya kuishi vyema na mwengine ulimwenguni (16-33). Mithali hizi zinajaribu kutuelekeza kwenye njia ya hekima katika viwango vitatu muhimu vya maisha: Mungu, mamlaka, na jamii yetu.

Mwishowe, tambua maudhui yanayojirudia ya ukuu wa Mungu katika mstari wa 1 na 9, na pia mstari wa 25 na 33. Cha msingi ni: "Usisahau!" mwandishi anatukumbusha, "Watu hupanga mipango mingi, lakini Mungu ndiye mwenye neno la mwisho."

Dag 16Dag 18

Om denne planen

BibleProject | Hekima ya Mithali

Kitabu cha Mithali kinasema kuwa hekima ya Mungu imedhihirishwa kupitia ulimwengu na unaalikwa kushiriki. Je, ni lipi chaguo la busara kuhusiana na pesa, kazi, uhusiano na shughuli za kimaisha za kila siku? Mwongozo huu wa siku 32 utakuwezesha kusoma kitabu cha Mithali hatua kwa hatua na kufahamu mwelekeo unaopaswa kuchukua.

More