BibleProject | Hekima ya MithaliPrøve
Sura ya 7: Ombi la Baba
Baba Anazungumza na Mwanawe Mara ya Kumi
Hii ni mara kumi na ya mwisho kwa baba kuzungumza na mwanawe, na mazungumzo haya yana hisia nzito kuliko awali. Baba amepiga magoti akimsihi mwanawe kuishi kwa hekima (na kuepuka mtego wa mwanamke mzinzi) kwa vyovyote vile. Tazama maneno ya vitendo yaliyotumika katika mstari wa 1-5. Haya yote yanahitaji bidii na kujitolea kabisa - "jitenge," "linda," "tunza," "zingatia", "andika," "sema," ita."
Kawaida, Kitabu cha Mithali hakina masimulizi, lakini katika mstari wa 6-20 baba anatumia simulizi kujieleza. Anamsimulia mwanawe simulizi ya kusikitisha kuhusu kijana asiye na busara ambaye ananaswa katika mtego wa mwanamke mzinzi. Maneno ya mwanamke huyo (mstari wa 14-20) yanavutia sana na anaonyesha urembo wake. Anatoa ahadi ya "kitanda chenye manukato" na "vitani vyenye rangi." Kijana huyu anamruhusu mwanake huyu mzinzi kumsifia, anakosa kutahadhari, na katika mstari wa 22 anashawishika. Baba anamlinganisha na ng'ombe dume, paa dume, na ndege, kwani wanyama hawa watatu hunaswa kwa urahisi.
Simulizi hii ya kina inakatika ghafla kwenye mstari wa 23, baba anapowageukia wanawe wote na kutoa ombi hili la mwisho (24-27): "Sikilizeni. Kwa. Yangu. Maneno," anasema, "Jiepusheni na mwanamke huyo!" Nyumba ya mwanamke mzinzi ni kaburi lililojificha, au kama anavyoeleza, "njia kuu kuelekea kaburini, inayokupeleka katika chemba za mautini."
Simulizi hii haikusudii kuzungumza na akili zetu tu; bali pia inazungumza na fikra na mioyo yetu. Baba angependa wanawe wasiyasahau aliyosema. Kuwa makini na madhara yake kwako.
Skriften
Om denne planen
Kitabu cha Mithali kinasema kuwa hekima ya Mungu imedhihirishwa kupitia ulimwengu na unaalikwa kushiriki. Je, ni lipi chaguo la busara kuhusiana na pesa, kazi, uhusiano na shughuli za kimaisha za kila siku? Mwongozo huu wa siku 32 utakuwezesha kusoma kitabu cha Mithali hatua kwa hatua na kufahamu mwelekeo unaopaswa kuchukua.
More