BibleProject | Hekima ya MithaliPrøve
Sura ya 8: Kushiriki Hekima ya Mungu
Binti Hekima Anazungumza Mara ya Tatu
Tofauti na uovu unaotongoza katika sura ya 7, sura ya 8 ni shairi zuri lililoandikwa na Binti Hekima kwa msomaji. Japo wanawake wote wawili wanatafuta wenza, mienendo yao ni tofauti sana. Mwanamke mzinzi anazungumza akiwa amejificha naye Binti Hekima anazungumza akiwa "juu" (mstari wa 2); mwanamke muovu hutumia maneno ya udanganyifu, lakini Hekima "huzungumza mazuri" (mstari wa 6). Tofauti hii inatumika ili tuvutiwe zaidi na mmoja wao na tujihadhari na yule wa pili.
Katika mstari wa 1-3 Binti Hekima anatambulishwa. Kwenye sehemu iliyosalia katika sura hii, anazungumza kwa ufasaha anachokileta mezani. Hotuba yake, hata hivyo, hayafanyiki penye hadhira. Badala yake, anatembea barabarani, akiwaita wale wenye ujasiri wa kusikiliza.
Shairi la Binti Hekima limejaa hisia na uzito. Ukilisoma litakushawishi. Lina urari, limejaa hisia na ushawishi. Katika mstari wa 4-21 anamsihi msomaji wake kuyasikiliza maneno ya kinywa chake, kwa kuwa ni bora kuliko fedha, dhahabu, au vito. Maneno yake pia hurithisha heshima: "Nina busara, Nina nguvu," anaahidi, "Kupitia mimi wafalme hutawala." Zaidi ya hayo, mstari wa 22-31 unarejelea historia na tunamwona Binti Hekima amesimama kando ya Muumbaji! Mungu alitumia hekima kuumba ulimwengu wetu mzuri na wa kipekee, na alifurahia kazi ya mikono Yake.
Ni nani anayeweza kulinganishwa na Binti Hekima?
Katika mstari wa 32-36 Binti Hekima anahitimisha shairi lake. Anazungumza na wana kama wake mwenyewe na kuwaambia "nitafuteni na mtapata uhai." Je, unatafuta Hekima "kila wakati"? Zingatia maneno yake kwa makini.
Skriften
Om denne planen
Kitabu cha Mithali kinasema kuwa hekima ya Mungu imedhihirishwa kupitia ulimwengu na unaalikwa kushiriki. Je, ni lipi chaguo la busara kuhusiana na pesa, kazi, uhusiano na shughuli za kimaisha za kila siku? Mwongozo huu wa siku 32 utakuwezesha kusoma kitabu cha Mithali hatua kwa hatua na kufahamu mwelekeo unaopaswa kuchukua.
More