BibleProject | Hekima ya MithaliPrøve

BibleProject | Hekima ya Mithali

Dag 3 av 32

Sura ya 2: Hekima na Kumfahamu Mungu

Baba akimzungumzia Mwanawe mara ya pili

Sura hii nzima ni baba akimzungumzia mwanawe mara ya pili. Ni mazungumzo ya kutoa mawaidha (hayataji sana adhabu) kama mazungumzo ya awali, lakini bado inasisitiza umuhimu wa kinachozungumziwa. Ukitafuta hekima utaipata, lakini unapaswa kuitafuta kwa bidii sana.

Mstari wa 4-5

"Tafuta [hekima] kama vile fedha na uitafute kama hazina zilizofichwa." Kwa kufanya hivyo utajua jinsi ya kumcha Bwana na utamfahamu Mungu.

Je, una hamu ya kupata hekima? Je, unaithamini kama kitu ambacho ni nadra na cha thamani? Ikiwa ni muhimu kwako, unapaswa kuitafuta kwa bidii kama mtu anayechimba dhahabu. Habari njema ni kuwa Mungu ni mkarimu katika kutoa hekima na mafanikio kwa wanaoyatafuta, hivyo kuwa tayari kutafuta hazina muhimu zaidi! Lakini tahadhari usiwe mwenye tamaa au kiburi: njia bora ya kufanikiwa ni kuwa mnyenyekevu na kuendelea kumwomba Mungu akusaidie.

Katika mstari wa 5 tunajifundisha kuwa "kumcha Mungu" ni sawa na kumjua Mungu. Kama mtoto anayegusa moto na kufahamu makali yake, tunapomfahamu Mungu, tunaheshimu kwa unyenyekevu uwezo Wake mkuu unaozidi vyote. Hii inabadilisha jinsi tunavyomwona, na pia tabia zetu. Huenda hili ni jambo zito kwako lakini usiwe na wasiwasi! Baba anaahidi kuwa hekima "inapoingia moyoni mwako," utapata mwelekeo na mwongozo, nayo maarifa "yatafurahisha nafsi yako."

Mstari wa 12-22: kuna taswira nyingi sana kuhusu njia ya mema au maovu. Baba anaonya kuhusu hatari mbili mahususi katika safari hii: utakumbana na watu ambao hutumia njia za mikato maishani kwa kuwadhulumu wengine (watu waovu), au watu wanaokutia katika majaribu ya kuvunja maagano yako ya ndoa kwa kushiriki ngono (mwanamke mzinzi). Watu hawa huenda wakakuvutia, lakini njia zao mbaya, potovu, yaani "njia za giza" zitakuletea taabu, au, kama asemavyo baba, "njia za mauti." Eeeeh! Kumbuka, hekima itakutenga mbali na mitego ya watu hawa na itakuongoza katika maisha ya utulivu na furaha.

Dag 2Dag 4

Om denne planen

BibleProject | Hekima ya Mithali

Kitabu cha Mithali kinasema kuwa hekima ya Mungu imedhihirishwa kupitia ulimwengu na unaalikwa kushiriki. Je, ni lipi chaguo la busara kuhusiana na pesa, kazi, uhusiano na shughuli za kimaisha za kila siku? Mwongozo huu wa siku 32 utakuwezesha kusoma kitabu cha Mithali hatua kwa hatua na kufahamu mwelekeo unaopaswa kuchukua.

More