BibleProject | Hekima ya MithaliPrøve

BibleProject | Hekima ya Mithali

Dag 2 av 32

Sura ya 1: Je, Hekima ina Umuhimu Gani?

Tuanze! Kabla hujasoma mithali zenyewe (kuanzia sura ya 10), utasoma sura tisa za mashairi. Lengo la mashairi haya ni kukupa hamu ya kufahamu jinsi hekima ya Mungu ilivyo muhimu katika maisha yako. Mashairi haya ni hotuba. Baadhi ya hotuba hizi ni baba akimzungumzia mwanawe. Mengine ni mazungumzo ya mhusika aitwaye "Binti Hekima" na zinazungumza na wewe moja kwa moja. Katika sura ya 1, wahusika hawa wawili wanazungumza.

Mstari wa 1-7: Utangulizi

Kabla ya mazungumzo haya, kuna utangulizi wa kitabu kizima. Kitabu hiki kinaanzia kwa mazungumzo mafupi kuhusu kusudi lake na ujumbe ni wazi: iwe unaamini umeyamudu au hujayamudu maisha yako, unahitaji ushauri huu. Utangulizi huu unaisha kwa kusema kuwa itakuwa vigumu kupata hekima usiponyenyekea chini ya mamlaka ya Mungu—"Kumcha Mungu," maudhui yanayojitokeza mara nyingi katika kitabu hiki. Maneno "Ni wapumbavu tu ambao hudharau maarifa na ufahamu," yanahitimisha mstari wa 7, na kuibua swali: "Utakuwa—Mwenye busara au mpumbavu?"

Mstari wa 8-9: Hotuba ya kwanza ya Baba akimzungumzia Mwanawe

Utangulizi unafuatiwa na hotuba, ya kwanza kati ya kumi, baba akimzungumzia mwanawe. Hapa baba anakashifu uovu kabisa, na anamwonya mwanawe bila kukwepesha kauli. Maneno yake ni mafupi, dhahiri na yenye uzito: watu wakijaribu kukushawishi ujinufaishe kirahisi kupitia njia "haramu" za mkato, usiwafuate. Kabisa Zitaleta uovu tu. Kabisa Baba anamalizia kwa kueleza kuhusu ukatili utakaotokana na kufuata njia hizi potovu (Dokezo: Anatumia neno damu SANA).

Mstari wa 20-33: Hotuba ya kwanza ya Binti Hekima

Usemi unaofuata ni hotuba ya kwanza kutoka kwa Binti Hekima, mhusika katika kitabu hiki anayehuisha dhana ya hekima. Anadai kwamba kukataa ushauri wake kutasababisha kijiangamiza na utajilaumu mwenyewe. Usipokuwa na hekima, utaangamia. Vibaya sana. Kimsingi, atakwambia"Nilikwambia" (Au kama anavyosema: "Matendo yako yatakufuata")

Kwa jumla, sura ya 1 inaweka hoja hii wazi: uamuzi wetu ni muhimu, lakini tunaweza kupata hekima. Kuna uwezekano wa kupotoka, lakini tuna mwongozo wa kutuelekeza. Chunga mienendo yako, kuwa mwangalifu na uzingatie uamuzi wako kwa makini. Je, uko tayari kusikiliza na kujifunza njia mpya za kuishi vyema katika ulimwengu wa Mungu? (Kidokezo: Kwa kweli unapaswa.)

Dag 1Dag 3

Om denne planen

BibleProject | Hekima ya Mithali

Kitabu cha Mithali kinasema kuwa hekima ya Mungu imedhihirishwa kupitia ulimwengu na unaalikwa kushiriki. Je, ni lipi chaguo la busara kuhusiana na pesa, kazi, uhusiano na shughuli za kimaisha za kila siku? Mwongozo huu wa siku 32 utakuwezesha kusoma kitabu cha Mithali hatua kwa hatua na kufahamu mwelekeo unaopaswa kuchukua.

More