BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 2 - Matendo ya MitumePrøve

BibleProject | Ufalme Unaoenda  Kinyume na Matarijio  / Sehemu ya 2 - Matendo ya Mitume

Dag 10 av 20

Baada ya Paulo na Barnaba kufukuzwa kutoka Antiokia, wanasafiri hadi jiji la Ikoniamu wakiwa na habari njema kuhusu Ufalme wa Yesu. Baadhi wanaamini ujumbe wao, lakini wale wanaoukataa wanaanzisha vurugu dhidi yao. Mambo yanakuwa magumu hadi jiji zima linagawanyika kuhusu suala hilo. Na wanafunzi wanapogundua kuna njama za kuwaua, wanahama na kwenda majiji ya Likaonia, Listra, Derbe, na maeneo ya karibu.

Wakiwa Listra, Paulo anakutana na mtu ambaye hajawahi kutembea. Paulo anapomponya kwa nguvu za Yesu, watu wanafikiri kimakosa kuwa Paulo ni mungu wa Kigiriki aliyekuja kuwatembelea, hivyo wanajaribu kumwabudu. Paulo na Barnaba wanawakosoa watu kwa haraka, wakisisitiza kuwa kuna Mungu mmoja tu wa kweli na wao ni watumishi wa huyo Mungu. Lakini watu hawaelewi kabisa, na wanashawishiwa haraka na maadui wa Paulo na Barnaba kuwa badala yake wanafaa kumuua Paulo. Wanampiga Paulo kwa mawe hadi anapoteza fahamu. Wanachukulia kuwa amekufa na kuburuza mwili wake nje ya Listra. Marafiki wa Paulo wanamzunguka na wanashangazwa pale anapoisimama na kutembea akirejea jijini. Siku inayofuata, Paulo na Barnaba wanatembelea Derbe ili kuhubiri Injili na wanarudi Listra na majiji ya karibu ili kuteua viongozi katika kila kanisa jipya na kuwatia moyo Wakristo kuvumilia katika shida.

Soma, Tafakari, kisha Ujibu:

• Ni nini kilikushangaza, kukutia wasiwasi, au kukustaajabisha ulivyosoma sura ya leo?

• Zingatia maneno ambayo mitume waliyasema ili kuimarisha makanisa (tazama 14:22). Umepitia shida gani katika maisha kwa sababu ya kumtegemea Yesu? Ujumbe huu unakutia moyo vipi leo?

• Badili kusoma kwako na tafakari yako kuwa maombi. Ongea na Mungu kuhusu kilichokusababishia kushangaa na jinsi unavyokubaliana na ujumbe wa Mungu. Kuwa mkweli kuhusu hofu zako na umwombe kile unachohitaji ili ustahimili.

Dag 9Dag 11

Om denne planen

BibleProject | Ufalme Unaoenda  Kinyume na Matarijio  / Sehemu ya 2 - Matendo ya Mitume

BibleProject ilibuni Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarajio Sehemu ya 2 ili kuwatia watu moyo, vikundi vidogo, na familia mbali mbali waweze kusoma Matendo ya Mitume kwa siku 20. Mpango huu unajumuisha video za katuni, mihtasari yenye mawazo yanayojenga, na maswali ya tafakari ili kuwasaidia washiriki kukutana na Yesu na kuzama kwenye ubunifu wa fasihi wa mwandishi na kuelewa na kujifunza kutoka kwenye mtiririko wa mawazo yake.

More