Soma Biblia Kila Siku 09/2024Mfano
Yehonadabu ametajwa katika Yer 35:5-10 na 18-19 kama mcha Bwana aliyeshika maagizo ya Mungu. Yeremia alipowawekea mabakuli yaliyojaa divai ili kujaribu uaminifu wa wana wa nyumba ya Warekabiwakasema, Hatutakunywa divai; kwa maana Yonadabu, mwana wa Rekabu, baba yetu, alituamuru, akisema, Msinywe divai, ninyi wala wana wenu, hata milele; … tukafanya sawasawa na yote aliyotuamuru Yonadabu, baba yetu.Kwa hiyoYeremia akawaambia watu wa nyumba ya Warekabi, Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Kwa sababu mmeitii amri ya Yonadabu, baba yenu, na kuyashika maagizo yake yote, na kutenda sawasawa na yote aliyowaamuru;basi, kwa sababu hiyo, Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Yonadabu, mwana wa Rekabu, hatakosa kuwa na mtu wa kusimama mbele zangu hata milele.Yehu akimkaribisha kwenye gari lake, anajitokeza kama mtu mwaminifu kwa Bwana. Lakini Yehu akikutana na watu wa dini ya Ubaali, anajitambulisha kama mcha Baali, ili kwa njia ya hila, udanganyifu na uuaji awafutilie mbali waabudu wote wa dini ya Yezebeli. Hata anabadilisha hekalu la Baali kuwa choo cha umma. Tafakari maana ya m.29 kwa maisha yako:Katika makosa yake Yeroboamu mwana wa Nebati, ambayo kwa hayo aliwakosesha Israeli, Yehu hakutoka katika kuyafuata, yaani, ndama za dhahabu zilizokuwako katika Betheli na Dani. Je, unamtumikia Bwana kwa moyo wako wote?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 09/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Tisa pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz