Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kuua Nguvu zinazoangamiza na John BevereMfano

Killing Kryptonite With John Bevere

SIKU 7 YA 7

Wito wa toba unaohitajika ndani ya na katoka kanisani leo ni wito wa kitu ambacho tunahitaji zaidi: upendo wa kweli. Ukosefu wa upendo wa kweli katika kanisa unajaza ibada zetu, huduma, na nyumba zetu na pande zote mbili—kuvumiliwa na Sheria.

Udanganyifu wa Kuvumiliwa ni kwamba unafanana sana na upendo. Tunatumia Biblia kufafanua upendo kuwa uvumilivu, fadhili, hauna wivu, una adabu, hautafuti mambo yake, pamoja na sifa nyinginezo zinazopatikana katika 1 Wakorintho 13. Hata hivyo, upendo wa dunia unaweza pia kuwa na baadhi ya sifa hizi. 

Kinachotenganisha Upendo wa Kikristo tofauti na upendo wa kidunia ni kwamba upendo wa Kikristo unatii amri za Mungu. “Hivi ndivyo tunavyojua,” anaandika mtume wa upendo, “Katika hili twajua kwamba twawapenda watoto wa Mungu, tumpendapo Mungu, na kuzishika amri zake.”‭‭1 Yoh.‬ ‭5:2‬ ‭

Hii inamaanisha kwamba, ikiwa mimi ni mvumilivu, sikosi adabu, sina wivu, sijivuni, lakini ninamfanyia uzinzi mke wangu ama ikiwa ninakubali uasherati, sitembei katika upendo wa Mungu. 

Upendo wa kweli unaashiriwa na sifa zote mbili: ukweli na upendo. Ukweli bila upendo unatuweka katika njia ya kusisitiza mambo madogomadogo ya sheria, ambayo inaua—uhalali. Aidha, cha kuhuzunisha, watu wanaitikia uhalali kwa kupeleka mzani upande mwingine, wanakataa kukosoa ama kutoa onyo kutoka kwenye maandiko, ambayo ni muhimu kwa afya na ukuzaji wa kanisa. 

Tuseme ukweli—tunaona kuita watu kwa toba ni ukosefu wa huruma, upole, hisani, na upendo. Lakini tafakari haya: Ikiwa ninamwona kipofu akielekea kwenye kilima ambapo ataanguka na kuangamia, upendo unanishurutisha nimwambie abadili njia yake!

Katika jamii yetu, na wengi wetu kanisani, upendo huo wa kweli unaoita watu kutubu unatazamiwa kuwa ubaguzi na chuki. Ngome hii imetokea kwa sababu tunafikiri kuhusu maisha yetu duniani pekee, wala si ya milele. 

Tunapokumbuka kwamba maisha haya ni mafupi sana yakilinganishwa na yajayo baadaye, tunaishi tofauti. Lazima tutazame maisha tukizingatia ya milele ili kuelewa upendo wa kweli. 

Huu ndio upendo ambao kanisa linahitaji wakati huu—upendo wa milele, upendo wa kweli—upendo utakaokabili dhambi na kuhimiza watu kutubu, ilhali bado pia upendo unaovumilia, wa hisani, na mpole.

Umefurahia mpango huu? Ninakuhimiza uchunguze zaidi kwa kusoma kitabu changu Killing Kryptonite.  

siku 6

Kuhusu Mpango huu

Killing Kryptonite With John Bevere

Kama Superman, ambaye anaweza kushinda kila adui, wewe kama mfuasi wa Kristo una uwezo wa kimiujiza kushinda changamoto unazopitia. Lakini shida yako na shida ya Superman ni kwamba nguvu zinazokudhoofisha zipo. Mpango huu utakusaidia kung'oa nguvu hizo maishani mwako, ili uweze kutimiza uwezo ambao Mungu alikupa na kuukumbatia maisha mwako bila mipaka. 

More

Tungependa kumshukuru John na Lisa Bevere (Messenger Int'l) kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: http://killingkryptonite.com