Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kuua Nguvu zinazoangamiza na John BevereMfano

Killing Kryptonite With John Bevere

SIKU 6 YA 7

Kuna mazingira ya aina tatu tofauti inapokuja suala la waumini na dhambi.

Kwanza, kuna wanaojiita waumini wanaopuuza dhambi kwa sababu wana mioyo migumu. Pili, kuna wanaojiita Wakristo wanaoamini uongo kwamba sisi sote ni wenye dhambi kiasili, kwamba damu ya Yesu ina nguvu ya kutuokoa kutokana na adhabu ya dhambi, lakini si utumwa wa dhambi. Vikundi hivi viwili, vinavyokabiliwa na dhambi, ni kama "nguvu ya kubadilisha" katika mwili wa Kristo, wakileta udhaifu katika mwili wote kwa sababu ya ukaidi wao wa kimakusudi kwa Kristo. 

Hata hivyo, kuna kikundi cha tatu—waumini wanaopambana na dhambi ili kuwa huru. Hiki ndicho kikundi ambacho ningependa kuzungumza nacho leo. 

Kitu cha kwanza ambacho ningependa kusema ni, Yesu hatawahi kuacha kukusamehe. Anaona mateso ambayo dhambi zako zinakuletea kila mara unapoanguka. Anajua kwamba una shauku kuu ya kuwa huru. Na kwa neema yake, maneno haya ya leo yanaweza kukusaidia. 

Nilikuwa katika kikundi hiki kwa miaka mingi kwa sababu ya kupenda ponografia. Nilikuwa napenda kwa miaka mingi kabla ya kuokoka na hata baada ya kuoa na kufanya kazi katika huduma, sikuweza kuwa huru. Niliwahi kuwa na mhubiri maarufu wa Marekani aIiweka mikono yake juu yangu na kuniombea ili niokolewe kutoka kwenye ulevi wangu. Haya yote yaliambulia patupu. 

Nilipata uhuru wangu nilipobadilisha yale mambo ambayo niliyapa kipaumbele. Mwanzoni, nilitaka Mungu aniachilie huru kwa sababu niliogopa kuwa dhambi yangu ingekuwa kizuizi katika huduma yangu. Lakini moyo wangu ukageuka, na nikaanza kuzingatia jinsi ambavyo maamuzi yangu yaliathiri uhusiano wangu na Yesu. Nikaanza kujali jinsi ambavyo dhambi yangu ilimwathiri Mungu. 

In 2 Wakorintho 7:10, Paulo anatofautisha aina mbili za huzuni—huzuni jinsi atakavyo Mungu ambayo huleta wokovu, na huzuni ya kidunia ambayo huleta kifo. Kisa changu kinadhihirisha huzuni hizo mbili. Mwanzoni, huzuni yangu ilikuwa ya kidunia, niliogopa ni nini ambacho kitatokea. Lakini baadaye, huzuni yangu ikawa ya kimungu, nilihangaishwa jinsi ambavyo dhambi yangu ilimwumiza Mungu na wengine. 

Rafiki mpendwa, nguvu ya Mungu ipo kukuweka huru kutokana na dhambi na kukupa maisha ya kimiujiza. Fuata toba ya kimungu, pokea msamaha wa Mungu, na uishi maisha yako mapya katika Kristo kwa ujasiri.

siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

Killing Kryptonite With John Bevere

Kama Superman, ambaye anaweza kushinda kila adui, wewe kama mfuasi wa Kristo una uwezo wa kimiujiza kushinda changamoto unazopitia. Lakini shida yako na shida ya Superman ni kwamba nguvu zinazokudhoofisha zipo. Mpango huu utakusaidia kung'oa nguvu hizo maishani mwako, ili uweze kutimiza uwezo ambao Mungu alikupa na kuukumbatia maisha mwako bila mipaka. 

More

Tungependa kumshukuru John na Lisa Bevere (Messenger Int'l) kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: http://killingkryptonite.com