Kuua Nguvu zinazoangamiza na John BevereMfano
Unakumbuka Angela katika somo la jana? Tulijifunza kwamba uzinzi wake ni sawa na jinsi ambavyo Biblia inaeleza ibada ya sanamu badala ya Mungu. Lakini hili ni tatizo katika kanisa la leo kwa kweli? Naam, cha kusikitisha ni kwamba bado ni tatizo.
Ukimtazama Angela, mzizi wa uzinzi wake ni hamu. Neno jingine la hamu ni kutamani.
Kutamani si jambo ambalo tunazungumzia mara nyingi siku hizi, kwa hivyo acha nilifafanue. Kulingana na Merriam-Webster, kutamani ni, “Hali ya kutaka sana kitu.” Acha nikupe mtazamo mwingine kuhusu kutamani kutoka Wakolosai 3:5, ambapo Paulo anasema, “ “Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu;”
Umeuona? Paulo anasema kwamba kutamani ni kuabudu sanamu! Pengine tunadhani kwamba ni kuinamia sanamu na vitu vinginevyo, lakini mzizi wa haya yote ni tamaa isiyo ya haki.
Mungu ametupa ufunguo ili kuondokana na tamaa, nao ni kuridhika. Kuridhika kunatutoa kwenye ibada ya sanamu na kutuweka karibu na moyo wa Mungu, ilhali tamaa inatutenga na Mungu na kutupeleka kwa madhabahu ya ibada ya sanamu.
Hii ndiyo maana mwandishi wa Waebrania anaandika, “ “Msiwe na tabia ya kupenda fedha; mwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa.” “Hata twathubutu kusema, Bwana ndiye anisaidiaye, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini?” (Waebrania 13:5–6).
Unaweza kutambua jinsi katika kifungu hiki ambavyo kutamani ni sawa na uzinzi. Angela alitamani wanaume wengine, hakumruhusu Justin kutosheleza mahitaji yake. Hapa tunaambiwa kuridhika na Mungu, tukijua atatosheleza mahitaji yetu yote. Tukifuata chanzo kingine nje ya Mungu na njia ambayo ametupa kuishi, huo ni kuabudu sanamu!
Maana ya hii ni kwamba: Muumini anapojua matakwa ya Mungu, lakini anachagua tamaa zake kimakusudi, hiyo ni ibada ya sanamu. Wamechagua kuabudu tamaa zao badala ya kumwabudu Mungu.
Ukitazama malengo, vipaumbele, na tabia zako, ni kipi unachoweza kusema kina nguvu zaidi maishani mwako—tamaa ama kuridhika? Ni vipi utafuata maisha ya kuridhika zaidi?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Kama Superman, ambaye anaweza kushinda kila adui, wewe kama mfuasi wa Kristo una uwezo wa kimiujiza kushinda changamoto unazopitia. Lakini shida yako na shida ya Superman ni kwamba nguvu zinazokudhoofisha zipo. Mpango huu utakusaidia kung'oa nguvu hizo maishani mwako, ili uweze kutimiza uwezo ambao Mungu alikupa na kuukumbatia maisha mwako bila mipaka.
More