Kuua Nguvu zinazoangamiza na John BevereMfano
Nakala ya Yahweh ilitokea vipi Israeli, na nakala ya Yesu inatokea vipi katika kanisa la leo? Zote mbili ni matokeo ya moyo ulio mgumu kwa sababu hakuna toba ya kweli.
Sasa, usiwe na wasiwasi. Ninajua kwamba toba imehubiriwa kwa njia ambayo inaleta utumwa, lakini hiyo si toba ya kibiblia. Ukweli ni kwamba tunahitaji toba, kwa sababu hatuwezi kushiriki katika maisha ambayo Mungu ametupangia bila toba.
Tukitazama yale ambayo Biblia inasema, tunapata kwamba karibu kila sauti ya Agano Jipya inasema wazi na mahususi kwamba toba ni sehemu ya lazima ya maisha yetu katika Kristo. Orodha ya watu ambao wanasema hivi waziwazi inajumuisha Petro, Paulo, Yohana, Yakobo, wafuasi wengine, Yesu mwenyewe, na hata Mungu Baba. Ni ukweli mkuu na ambao bila shaka ni dhahiri.
Hii inamaanisha kwamba hakuna imani ya kweli katika Yesu Kristo bila toba ya dhambi zinazojulikana. Na dhambi ni nini? Dhambi ni kinyume cha mambo bora ambayo Mungu ametutakia.
Hii inamaanisha kwamba hatuwezi kuja kwa Yesu ikiwa tunakataa kuasi vitu kama uasherati, kusengenya, na kutosamehe.
Utasemaje kwamba wewe ni Mkristo na unaendelea kushikilia hivi vitu? Ukweli ni kwamba, kuna amri zaidi ya mia tano zinazohusu tabia katika Agano Jipya. Mungu anatupa amri hizi kwa sababu hawezi kustahimili vitu ambavyo vinaweza kukuangamiza—anakupenda sana.
Lakini ikiwa tutashikilia dhambi ambazo Kristo alitufia ili kutuokoa, tumeunda nakala ya Yesu, na imani yetu ni jambo ambalo tumebuni.
Toba ya kibiblia ni kitendo kikuu zaidi cha unyenyekevu, kufungua maisha yetu kuruhusu maajabu ya neema ya Mungu maishani mwetu. Kwa kweli, Mungu anaapa kutupa neema tukinyenyekea (Yakobo 4, 1 Petro 5). Hii ndiyo maana toba ni muhimu sana . . . hatuwezi kuaibika kwa ajili yake. Ni lazima wanaotafuta na wanaojiita waumini wajue haya. Ni lazima kwa imani na wokovu wetu!
Toba inamaanisha kubadili maisha yetu kwa undani hadi utu unabadilika kutoka kwenye kiini cha uhai wetu. Tunapomfuata Yesu anatufanya upya, akitupa neema kuishi kama yeye.
Hii ni toba ya kibiblia—ni hatua ya kuundwa upya katika Kristo, ukiangaza wema na asili ya Mungu kwa ulimwengu. Pana mwaliko mkuu zaidi?
Kuhusu Mpango huu
Kama Superman, ambaye anaweza kushinda kila adui, wewe kama mfuasi wa Kristo una uwezo wa kimiujiza kushinda changamoto unazopitia. Lakini shida yako na shida ya Superman ni kwamba nguvu zinazokudhoofisha zipo. Mpango huu utakusaidia kung'oa nguvu hizo maishani mwako, ili uweze kutimiza uwezo ambao Mungu alikupa na kuukumbatia maisha mwako bila mipaka.
More