Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kuua Nguvu zinazoangamiza na John BevereMfano

Killing Kryptonite With John Bevere

SIKU 2 YA 7

Jioni mmoja, Justin anarudi nyumbani kutoka kazini na kumkuta mke wake, Angela, amejipodoa na akivaa nguo maridadi. Anafikiria kwamba lazima amewapanga kitu maalum kwa ajili yaona ameamua kujipamba pia. 

Angela, akiwa amechanganyikiwa kidogo, anajibu, “Mpenzi, ninakutana na Tony usiku huu. Tutakula chakula cha jioni, kisha kutazama filamu, na mwishowe tutaenda Hoteli ya Fairmont. Nitarudi pengine saa nne asubuhi.” 

“Tony ni nani?!” Justin anamwuliza.

“Alikuwa mpenzi wangu kutoka shule ya Sekondari,” alisema.

“Nini! Huwezi kutoka naye!” 

“Kwa nini?” 

“Kwa sababu tumeoana; tumejiweka wakfu. Hatutoki na watu wengine!” anasema, akitoa kauli ambayo anadhani inaonekana wazi.

“Subiri kidogo, mpenzi!” Angela anamjibu. “Ninakupenda kuliko mpenzi yeyote wa zamani, lakini huwezi kutarajia kwamba sitawaona tena. Tumekuwa karibu na wengi wao kwa miaka mingi, bado nawapenda, na ninataka kujiburudisha nao. Nini kibaya kwa hilo?”

Bila shaka hawa si wanandoa wa kweli. Hatuwezi hata kuwaza kwamba mtu haelewi kwamba ndoa inamaanisha uhusiano usiowahusisha wengine. Kwa hakika, hakuna mtu miongoni mwetu angeoa mtu kama Angela ambaye anatarajia kuendelea kukutana na wapenzi wake wa zamani.

Lakini hivi ndivyo wengi wetu wanafanya katika uhusiano wetu na Yesu. 

Katika Maandiko yote, Mungu analinganisha uhusiano wake nasi kwa uhusiano wa ndoa. Aidha ni jinsi ambavyo Mungu alizungumza kuhusu uhusiano wake na Israeli katika Agano la Kale. Ya kuvutia ni kwamba, kila mara Mungu alizungumza na Israeli kupitia manabii kuhusu jinsi ambavyo walikuwa wametenda uzinzi kinyume naye, ilihusu suala la ibada ya sanamu. 

Pengine tunadhani kwamba ibada ya sanamu ni kuinamia sanamu, lakini kiini chake ni ibada. Mungu anafafanua ibada inapotajwa kwa mara ya kwanza katika Maandiko, katika hadithi ya Ibrahimu na Isaka. Hapa, tunaona kwamba ibada ni utii. 

Ibada si wimbo unaovuti wa mtindo wa taratibu; ni utii. Haijalishi jinsi ambavyo “tunahudumu” kanisa, ikiwa hatumtii Mungu katika maisha yetu ya kila siku, hatumwabudu bali, kwa uhakika, tunaishi kwa uzinzi kama Angela. 

Ufahamu huu wa ibada unabadili vipi fikra zako kuhusu maisha ya Kikristo? 

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Killing Kryptonite With John Bevere

Kama Superman, ambaye anaweza kushinda kila adui, wewe kama mfuasi wa Kristo una uwezo wa kimiujiza kushinda changamoto unazopitia. Lakini shida yako na shida ya Superman ni kwamba nguvu zinazokudhoofisha zipo. Mpango huu utakusaidia kung'oa nguvu hizo maishani mwako, ili uweze kutimiza uwezo ambao Mungu alikupa na kuukumbatia maisha mwako bila mipaka. 

More

Tungependa kumshukuru John na Lisa Bevere (Messenger Int'l) kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: http://killingkryptonite.com