Soma Biblia Kila Siku 02/2024Mfano
Sheria ya jino kwa jino ilikuwa ni mwongozo kwa watoa hukumu kama mahakimu na majaji. Kulipiza kisasi si haki. Adhabu hutolewa kulingana na uzito wa kosa. Lengo la adhabu ni kuzuia matendo ya kikatili na kishenzi katika mahusiano yetu. Yesu anatumia kanuni hii ya adhabu kutufundisha tusitendeane ovu kwa ovu (ukiwa na nafasi, soma Yesu anavyosema katika Mt 5:38-48). Hivyo, wote wanaohusika na kutoa maamuzi wanapaswa kuomba hekima kabla ya kutoa hukumu juu ya wakosaji. Adhabu bora ni ile inayolenga kurekebisha na kuokoa na si kuangamiza.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 02/ 2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/