Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kut 21:28-36

Kut 21:28-36 SUV

Ng’ombe akipiga pembe mtu mume au mtu mke, nao wakafa, huyo ng’ombe atauawa kwa kupigwa kwa mawe, nyama yake isiliwe; lakini mwenye huyo ng’ombe ataachiliwa. Lakini kwamba huyo ng’ombe alizoea kupiga watu tangu hapo, naye mwenyewe ameonyeshwa jambo hilo, wala asimzuie, naye amemwua mtu mume au mwanamke; huyo ng’ombe atauawa kwa kupigwa kwa mawe, na huyo mwenyewe naye atauawa. Lakini akiandikiwa ukombozi, ndipo atakapotoa kwa ajili ya uhai wake hicho atakachoandikiwa. Akiwa ng’ombe amempiga pembe mtoto wa kiume na kumtumbua, au akiwa amempiga mtoto wa kike, atatendwa kama hukumu hiyo. Ng’ombe akimtumbua mtumwa mume au kijakazi; mwenye ng’ombe atampa bwana wao shekeli thelathini za fedha, naye ng’ombe atauawa kwa kupigwa kwa mawe. Kwamba mtu atafunua shimo, au kuchimba shimo, naye asilifunike, kisha ikawa ng’ombe au punda kutumbukia humo, mwenye shimo atalipa; atampa huyo mwenye mnyama fedha, na mnyama aliyekufa atakuwa ni wake. Ng’ombe wa mtu akimwumiza ng’ombe wa mtu mwingine hata akafa; ndipo watamwuza huyo ng’ombe aliye hai na kugawanya thamani yake; na ng’ombe aliyekufa pia watamgawanya. Au kwamba ilijulikana ya kuwa ng’ombe tangu hapo amezoea kupiga kwa pembe, wala mwenyewe asimzuie; ndipo atakapolipa yeye, ng’ombe kwa ng’ombe, na huyo ng’ombe aliyekufa atakuwa ni wake.