Kutoka 21:28-36
Kutoka 21:28-36 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ng’ombe akipiga pembe mtu mume au mtu mke, nao wakafa, huyo ng’ombe atauawa kwa kupigwa kwa mawe, nyama yake isiliwe; lakini mwenye huyo ng’ombe ataachiliwa. Lakini kwamba huyo ng’ombe alizoea kupiga watu tangu hapo, naye mwenyewe ameonyeshwa jambo hilo, wala asimzuie, naye amemwua mtu mume au mwanamke; huyo ng’ombe atauawa kwa kupigwa kwa mawe, na huyo mwenyewe naye atauawa. Lakini akiandikiwa ukombozi, ndipo atakapotoa kwa ajili ya uhai wake hicho atakachoandikiwa. Akiwa ng’ombe amempiga pembe mtoto wa kiume na kumtumbua, au akiwa amempiga mtoto wa kike, atatendwa kama hukumu hiyo. Ng’ombe akimtumbua mtumwa mume au kijakazi; mwenye ng’ombe atampa bwana wao shekeli thelathini za fedha, naye ng’ombe atauawa kwa kupigwa kwa mawe. Kwamba mtu atafunua shimo, au kuchimba shimo, naye asilifunike, kisha ikawa ng’ombe au punda kutumbukia humo, mwenye shimo atalipa; atampa huyo mwenye mnyama fedha, na mnyama aliyekufa atakuwa ni wake. Ng’ombe wa mtu akimwumiza ng’ombe wa mtu mwingine hata akafa; ndipo watamwuza huyo ng’ombe aliye hai na kugawanya thamani yake; na ng’ombe aliyekufa pia watamgawanya. Au kwamba ilijulikana ya kuwa ng’ombe tangu hapo amezoea kupiga kwa pembe, wala mwenyewe asimzuie; ndipo atakapolipa yeye, ng’ombe kwa ng’ombe, na huyo ng’ombe aliyekufa atakuwa ni wake.
Kutoka 21:28-36 Biblia Habari Njema (BHN)
“Ngombe akimpiga mtu pembe na kumwua, ng'ombe huyo atauawa kwa kupigwa mawe na nyama yake haitaliwa. Mwenye ng'ombe huyo hatakuwa na lawama. Lakini kama ng'ombe huyo amezoea kupiga watu pembe, na mwenyewe akaonywa lakini hakumfunga, kama ng'ombe huyo akiua mtu lazima apigwe mawe, na mwenyewe lazima auawe. Hata hivyo, huyo mtu akitozwa faini ili kuyaokoa maisha yake, ni lazima alipe kiasi kamili atakachotozwa. Ngombe akimpiga pembe mtoto wa mtu mwingine, shauri hili litaamuliwa kwa njia hiyohiyo. Kama ng'ombe huyo akimpiga pembe mtumwa wa kiume au wa kike, mwenye ng'ombe atamlipa bwana wa huyo mtumwa fedha zenye thamani ya shekeli thelathini, na huyo ng'ombe lazima auawe kwa kupigwa mawe. “Mtu akiacha shimo wazi, ama akichimba shimo kisha asilifunike, halafu ng'ombe au punda akatumbukia humo, huyo mwenye shimo hilo lazima atoe fidia; atamlipa mwenye mnyama huyo fedha, na mnyama aliyekufa atakuwa wake. “Ngombe wa mtu akimwumiza ng'ombe wa mtu mwingine na kumwua, basi, watu watamwuza huyo ng'ombe aliyebaki hai na kugawana bei yake; vilevile watagawana yule ng'ombe aliyekufa. Lakini kama huyo ng'ombe alikuwa amezoea kupiga wengine pembe na mwenyewe hakumfunga, mwenyewe atalipa ng'ombe kwa ng'ombe, na yule aliyeuawa atakuwa wake.
Kutoka 21:28-36 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ng'ombe akimpiga pembe mwanamume au mwanamke, nao wakafa, huyo ng'ombe atauawa kwa kupigwa kwa mawe, nyama yake isiliwe; lakini mwenye huyo ng'ombe ataachiliwa. Lakini kama huyo ng'ombe alizoea kupiga watu tangu hapo, naye mwenyewe ameoneshwa jambo hilo, wala asimzuie, naye amemwua mwanamume au mwanamke; huyo ng'ombe atauawa kwa kupigwa kwa mawe, na huyo mwenyewe naye atauawa. Lakini akiandikiwa ukombozi, ndipo atakapotoa kwa ajili ya uhai wake hicho atakachoandikiwa. Akiwa ng'ombe amempiga pembe mtoto wa kiume na kumtumbua, au akiwa amempiga mtoto wa kike, atatendwa kama hukumu hiyo. Ng'ombe akimtumbua mtumwa mume au kijakazi; mwenye ng'ombe atampa bwana wao shekeli thelathini za fedha, naye ng'ombe atauawa kwa kupigwa kwa mawe. Ikiwa mtu atafunua shimo, au kuchimba shimo, naye asilifunike, kisha ikawa ng'ombe au punda kutumbukia humo, mwenye shimo atalipa; atampa huyo mwenye mnyama fedha, na mnyama aliyekufa atakuwa ni wake. Ng'ombe wa mtu akimwumiza ng'ombe wa mtu mwingine hata akafa; ndipo watamwuza huyo ng'ombe aliye hai na kugawanya thamani yake; na ng'ombe aliyekufa pia watamgawanya. Au ikiwa ilijulikana ya kuwa ng'ombe tangu hapo amezoea kupiga kwa pembe, wala mwenyewe asimzuie; ndipo atakapolipa yeye, ng'ombe kwa ng'ombe, na huyo ng'ombe aliyekufa atakuwa ni wake.
Kutoka 21:28-36 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ng’ombe akipiga pembe mtu mume au mtu mke, nao wakafa, huyo ng’ombe atauawa kwa kupigwa kwa mawe, nyama yake isiliwe; lakini mwenye huyo ng’ombe ataachiliwa. Lakini kwamba huyo ng’ombe alizoea kupiga watu tangu hapo, naye mwenyewe ameonyeshwa jambo hilo, wala asimzuie, naye amemwua mtu mume au mwanamke; huyo ng’ombe atauawa kwa kupigwa kwa mawe, na huyo mwenyewe naye atauawa. Lakini akiandikiwa ukombozi, ndipo atakapotoa kwa ajili ya uhai wake hicho atakachoandikiwa. Akiwa ng’ombe amempiga pembe mtoto wa kiume na kumtumbua, au akiwa amempiga mtoto wa kike, atatendwa kama hukumu hiyo. Ng’ombe akimtumbua mtumwa mume au kijakazi; mwenye ng’ombe atampa bwana wao shekeli thelathini za fedha, naye ng’ombe atauawa kwa kupigwa kwa mawe. Kwamba mtu atafunua shimo, au kuchimba shimo, naye asilifunike, kisha ikawa ng’ombe au punda kutumbukia humo, mwenye shimo atalipa; atampa huyo mwenye mnyama fedha, na mnyama aliyekufa atakuwa ni wake. Ng’ombe wa mtu akimwumiza ng’ombe wa mtu mwingine hata akafa; ndipo watamwuza huyo ng’ombe aliye hai na kugawanya thamani yake; na ng’ombe aliyekufa pia watamgawanya. Au kwamba ilijulikana ya kuwa ng’ombe tangu hapo amezoea kupiga kwa pembe, wala mwenyewe asimzuie; ndipo atakapolipa yeye, ng’ombe kwa ng’ombe, na huyo ng’ombe aliyekufa atakuwa ni wake.
Kutoka 21:28-36 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
“Fahali akimuua mwanaume au mwanamke kwa kumpiga kwa pembe, fahali huyo ni lazima auawe kwa kupigwa mawe, na nyama yake haitaliwa. Lakini mwenye fahali huyo hatawajibika. Lakini hata hivyo, ikiwa huyo fahali amekuwa na tabia ya kupiga kwa pembe, na mwenyewe ameonywa na hakutaka kumfungia naye akamuua mwanaume au mwanamke, huyo fahali ni lazima auawe kwa mawe na mwenye fahali pia auawe. Lakini ikiwa malipo yatatakiwa kwake, basi anaweza kulipa kinachodaiwa ili kuukomboa uhai wake. Sheria hii pia itatumika ikiwa fahali atampiga kwa pembe mwana au binti. Fahali akimpiga mtumwa wa kike au wa kiume, mwenye fahali atalipa shekeli thelathini za fedha kwa bwana mwenye mtumwa, na fahali ni lazima auawe kwa mawe. “Mtu akiacha shimo wazi, ama akachimba shimo kisha asilifukie, na ng’ombe au punda akatumbukia ndani yake, mwenye shimo ni lazima alipe hasara iliyotokea; ni lazima amlipe mwenye mnyama. Mnyama aliyekufa atakuwa wake. “Fahali wa mtu fulani akimuumiza fahali wa mtu mwingine na akafa, watamuuza yule aliye hai na wagawane sawa fedha pamoja na mnyama aliyekufa. Hata hivyo, ikifahamika kwamba fahali huyo alikuwa na tabia ya kupiga kwa pembe na mwenyewe hakumfunga, ni lazima mwenye fahali alipe mnyama kwa mnyama, na mnyama aliyekufa atakuwa wake.