Soma Biblia Kila Siku 02/2024Mfano
Katika Kut 20:16 imeandikwa,Usimshuhudie jirani yako uongo. Kusema uongo ni sumu inayoua tabia ya msemaji na anayesemwa. Mambo kama migongano, migogoro, vita, na kukosa maelewano yanachangiwa na kuwepo kwa uongo na wasema uongo. Mungu anachukia tabia ya kuneneana isivyo haki, na anaagiza isiwepo. Hivyo, wewe ujifunze kuacha tabia ya kusengenya. Badala yake, ujifunze kulinda heshima na sifa ya wengine ili isiharibike. Umtendee mema adui yako. Umtetee mnyonge, na epukana na ufisadi. Tafuta kukumbuka na kufuata 1 The 5:15,Angalieni mtu awaye yote asimlipe mwenziwe mabaya kwa mabaya; bali siku zote lifuateni lililo jema, ninyi kwa ninyi na kwa watu wote.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 02/ 2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/