Soma Biblia Kila Siku 02/2024Mfano
Amri za 4-10 ni sehemu ya pili ya amri 10. Fungu hili linahusu namna ya kuhusiana miongoni mwetu wanadamu. Zinahusu uhusiano kati ya mtoto na wazazi, na jinsi ya kutendeana bila kudhuriana. Mungu anatuagiza tuhusiane na yeye kwanza, ndipo tuhusiane na wenzetu. Uhusiano huu unahusu jinsi itupasavyo kutenda katika kupendana, kuheshimiana, kutunza wenzi na kutunza mali za jirani, kanisa na zile za taifa. Jinsi amri hizi mbili zinavyokwenda pamoja, Yesu anaeleza wazi katika Mk 12:29-31,Ya kwanza ndiyo hii, Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja; nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote.Na ya pili ndiyo hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi. Amri zote zinalenga kumwongoza mtu ili aishi maisha ya utakatifu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 02/ 2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/