Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku /Novemba 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku /Novemba 2023

SIKU 25 YA 29

Mungu hapendi watu waishi watakavyo. Kwa hiyo waliopuuza maagizo ya Mungu hawakupata chakula siku ya saba, ili wajifunze kuyafuata:Ikawa siku ya saba wengine wakatoka kwenda kukiokota, wasikione.Bwana akamwambia Musa, Mtakataa kuyashika maagizo yangu na sheria zangu hata lini?(m.27-28). Kufanya kazi ni lazima, lakini vilevile kupumzika ni lazima. Waliagizwa waweke ukumbusho ili wasilisahau tukio hili kwamba muda wote wa kusafiri Mungu aliwaandalia chakula cha mana. Maisha yao yote ya jangwani yalitegemea lisho la Mungu. Kwetu, Yesu Kristo ndiye chakula cha uzima kitokacho mbinguni muda wote tukiishi hapa duniani. Tafakari Yesu alivyofafanua habari hizo kwa Wayahudi:Baba zetu waliila mana jangwani kama vile ilivyoandikwa, Aliwapa chakula cha mbinguni ili wale. … Amin, amin, nawaambieni, Siye Musa aliyewapa chakula kile cha mbinguni, bali Baba yangu anawapa ninyi chakula cha kweli kitokacho mbinguni. Kwa maana chakula cha Mungu ni kile kishukacho kutoka mbinguni na kuupa ulimwengu uzima. Basi wakamwambia, Bwana, sikuzote utupe chakula hiki(Yn 6:31-35).

siku 24siku 26

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku /Novemba 2023

Soma Biblia Kila Siku /Novemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Novemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka na Warumi. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/