Soma Biblia Kila Siku /Novemba 2023Mfano
Mungu anaingilia na kuondoa majanga yanayoisibu jamii, akililisha taifa la Israeli kwa chakula wasichofanyia kazi. Katika m.12-13 anasema,Nimeyasikia manung'uniko ya wana wa Israeli; haya sema nao, ukinena, Wakati wa jioni mtakula nyama, na wakati wa asubuhi mtashiba mkate; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.Ikawa wakati wa jioni, kware wakakaribia, wakakifunikiza kituo; na wakati wa asubuhi umande ulikuwa juu ya nchi pande zote za kituo. Sasa Mungu ni wa utaratibu. Amri ya uumbaji izingatiwe. Kuna siku za kazi na siku ya kupumzika.Siku sita mtaokota; lakini siku ya saba ni Sabato, siku hiyo hakitapatikana(m.26). Msingi wa habari hiyo unapatikana katika amri katika Kut 20:9-10:Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote;lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako.Hivyo Mungu anawapa chakula cha siku moja tu, ila siku ya sita wakusanye pia kwa ajili ya siku ya saba. Woga unawasumbua, ila kwa vitendo wanajifunza kuweka tumaini kwa Mungu. Hii itukumbushe kufanya vivyo hivyo. Mungu anajua kesho yako.Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake(Mt 6:34).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku /Novemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Novemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka na Warumi. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/