Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku /Juni 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku /Juni 2023

SIKU 22 YA 30

Hatujui huyu nabii ni nani, lakini si Eliya. Walikuwepo manabii wengine wacha Mungu. Katika vita hii Mungu anajidhihirisha tena kwa Ahabu. Lengo la Mungu ni kwamba Ahabu atambue kuwa Mungu ni Bwana. Ahabu anasikiliza maneno ya nabii na kushinda katika vita, pia anasaidiwa kwa kutabiriwa ajiandae kwa vita itakayotokea mwaka ujao. Lakini bado Ahabu hajatambua ukuu wa Mungu. Zingatia onyo analotoa Paulo katika Rum 2:4-5 akiuliza,Waudharau wingi wa wema wake na ustahimili wake na uvumilivu wake, usijue ya kuwa wema wa Mungu wakuvuta upate kutubu? Bali kwa kadiri ya ugumu wako, na kwa moyo wako usio na toba, wajiwekea akiba ya hasira kwa siku ile ya hasira na ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu. Wewe je,waudharau wingi wa wema wake na ustahimili wake na uvumilivu wake Mungu?

siku 21siku 23

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku /Juni 2023

Soma Biblia Kila Siku Juni 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Matendo ya Mitume, Filemoni na 1 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu.

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/