Soma Biblia Kila Siku /Juni 2023Mfano
Wakati waamini wakiingojea ile ahadi juu ya Roho Mtakatifu ulikuwa ni wakati wa Wayahudi kusherekea sikukuu ya mavuno. Ilifanyika siku 50 baada ya Pasaka (maana ya "pentekoste" ni "hamsini"). Lakini mwaka huo yalitukia mambo tofauti sana. Na siku hiyokukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi. Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao(m.2-4). Walinena kwa lugha mpya ambazo zilikuwa na maana kwa wasikiaji. Watu walisikia kwa lugha zao matendo makuu ya Mungu aliyoyatenda. Bado Roho Mtakatifu yupo na kutuwezesha kutangaza kwamba kila anayemwomba Yesu amwokoe ataokolewa.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Juni 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Matendo ya Mitume, Filemoni na 1 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/