Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku /Juni 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku /Juni 2023

SIKU 5 YA 30

Bila kulishika na kulihubiriNeno la Mungukanisa litakufa au litadanganyika na kubadilika kuwa kanisa la uongo. Angalia kwa makini jinsi Petro alivyokuwa na msimamo katika neno la Mungu. Anayowaambia watu nimambo yale aliyohubiri Mungu tangu zamani kwa kinywa cha manabii wake wote, ya kwamba Kristo wake atateswa, ameyatimiza hivyo(m.18). Kwa hiyo muujiza ule ukampa Petro nafasi ya kuhubiri neno la Mungu na kumtukuza Kristoambaye ninyi[Wayahudi]mlimsaliti na kumkana mbele ya Pilato … mkamwua yule Mkuu wa uzima, ambaye Mungu amemfufua katika wafu; na sisi tu mashahidi wake(m.13-15). Je, ndivyo inavyotendeka Tanzania leo? Kumbuka Yesu alivyosema,Kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba(Mt 7:24).

siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku /Juni 2023

Soma Biblia Kila Siku Juni 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Matendo ya Mitume, Filemoni na 1 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu.

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/