Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku /Juni 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku /Juni 2023

SIKU 10 YA 30

Ni matukio makubwa ya ajabu yaliyotendeka katika kanisa la kwanza!1.Walioamini wakazidi kuongezeka kwa Bwana, wengi, wanaume na wanawake(m.14)!2.Wote wakaponywa,yaani wote waliokujakuombauponyaji wakiwa wagonjwa wa kawaida au wenye mapepo (m.16)!3.Malaika wa Bwana akafungua milango ya gereza, akawatoa ... wakaenda alfajiri hekaluni, wakaanza kufundisha(m.19 na 21). Haya ni matokeo ya watu wa Mungu kuamua kwa pamoja kuomba jambo fulani. Kwa umoja Petro na Yohana waliomba:Basi sasa, Bwana, yaangalie matisho yao; ukawajalie watumwa wako kunena neno lako kwa ujasiri wote, ukinyosha mkono wako kuponya; ishara na maajabu vifanyike kwa jina la Mtumishi wako mtakatifu Yesu. Hata walipokwisha kumwomba Mungu, mahali pale walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri(Mdo 4:29-31).

siku 9siku 11

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku /Juni 2023

Soma Biblia Kila Siku Juni 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Matendo ya Mitume, Filemoni na 1 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu.

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/