Soma Biblia Kila Siku /Juni 2023Mfano
Kuna wakati ambapo umekuwa mgumu sana katika maisha yako, wakati ambapo uliona huna msaada hata katika wito wako. Ukaogopa sana ukaona maadui ni wengi sana na ukaogopa hata kuwaambia, ni kama ni wakati ulitembea gizani katika hofu nyingi. Kumbe wakati kama huo ndiyo wakati wa kumtumaini Bwana Yesu na kumwomba yeye na kumsifu, kwani yeye ni nuru, mwamba na wokovu wako. Mtunga Zaburi anasema,Neno Moja nimelitaka kwa Bwana, … Nikae nyumbani mwa Bwana … Niutazame uzuri wa Bwana(m.4).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Juni 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Matendo ya Mitume, Filemoni na 1 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/