Soma Biblia Kila Siku /Juni 2023Mfano
![Soma Biblia Kila Siku /Juni 2023](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F37783%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Haiwezekani kuondoa utumwa kwa kupitishasheriatu, lakiniInjiliyamfanya bwana na mtumwa wake kuwa ndugu. Kwa hiyo kwa unyenyekevu Paulo anamsihi Filemoni amsamehe mtumwa wake, Onesimo, na kumpokea kama ndugu, si kwa kulazimika bali kwa hiari. Onesimo alikuwa amemtoroka Filemoni baada ya kufanya makosa, akakimbilia Rumi. Huko akakutana na Paulo, na alipohubiriwa Injili, hiyo ikabadilisha maisha yake. Sasa Paulo anaomba Onesimo aendelee kuwa mtumishi wa Injili. Unafikiri Filemoni alijibuje?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
![Soma Biblia Kila Siku /Juni 2023](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F37783%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Soma Biblia Kila Siku Juni 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Matendo ya Mitume, Filemoni na 1 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/