Soma Biblia Kila Siku /Juni 2023Mfano
Ingawa Ahabu hakutubu, Mungu anampa nafasi nyingine ya kuona utukufu wa Bwana, Mungu wa Israeli. Mfalme mgeni Ben-hadadi alikuwa amewaunganisha wafalme thelathini na wawili kupiga vita dhidi ya Ahabu. Kwanza Ahabu anakubali madai yao kuhusu mali yake . Lakini madai yakiongezeka, Ahabu pamoja na wenzake wanakataa kutawaliwa na Ben-hadadi kama mithali ya Mfalme katika m.11 inavyoonyesha. Hapo Ahabu anatuma ujumbe unaosema,Mwambieni, Avaaye asijisifu kama avuaye. Lakini hatusikii kwamba Ahabu alitafuta msaada wa Mungu, wala hakumlilia Mungu katika shida hii.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Juni 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Matendo ya Mitume, Filemoni na 1 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/