Soma Biblia Kila Siku /Juni 2023Mfano
Kila kabila liwe na urithi wake. Ni amri ya Mungu kwa Waisraeli kuhusu urithi wa ardhi. Amri hii inaeleza kwambahapana urithi wo wote wa wana wa Israeli utakaotoka kabila hii kwenda kabila hii; kwa kuwa wana wa Israeli watashikamana kila mtu na urithi wa kabila ya baba zake(Hes 36:7). Tena,atakayelikufuru jina la Bwana hakika atauawa(Law 24:16), na lazima wawepo mashahidi wasipungue wawili;asiuawe kwa mdomo wa shahidi mmoja(Kum 17:6). Ahabu na viongozi wenzake walijaa uovu. Hawakufuata neno la Mungu, bali walitumia ujanja ili kumwondoa Nabothi. Habari hii ni kama unabii juu ya viongozi walivyomhukumu Yesu, Mwana wa Mungu. Walipomwonawakasemezana wao kwa wao, Huyu ni mrithi; haya na tumwue, tuutwae urithi wake. Wakamkamata, wakamtupa nje ya shamba la mizabibu, wakamwua(Mt 21:38-39). Hutokea katika nchi ambapo mioyo ya wenye mamlaka imejaa uovu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Juni 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Matendo ya Mitume, Filemoni na 1 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/