Soma Biblia Kila Siku /Juni 2023Mfano
Imepita miaka mitatu tu tangu Ahabu alipomhurumia Ben-hadadi na kupatana naye, na sasa mfalme wa Shamu anataka kumwondoa Ahabu, yeye tu. Anawaelekeza wapiganajiakisema, Msipigane na mdogo wala mkuu, ila na mfalme wa Israeli peke yake(m.31). Wakati huu Mungu hayupo upande wa Ahabu tena. Anauawa kwa mshale uliorushwa kwa kubahatisha tu, yaani baadaye hata adui hakuweza kujisifu kitu.Ndipowakaliosha gari penye birika la Samaria, na mbwa wakaramba damu yake; sawasawa na neno la Bwana alilolinena(m.38).Huu ni uthibitisho kwamba neno la Mungu lilitimia kikamilifu. Vilevile ilitimia kama Mungu alivyomtangazia Ahabu katika 21:29,Kwa sababu[Ahabu]amejidhili mbele yangu, sitayaleta yale mabaya katika siku zake; ila katika siku za mwanawe nitayaleta mabaya hayo juu ya nyumba yake. Mfalme Ahabu alikufa kabla adhabu yote ya Mungu haijatekelezwa juu ya ukoo wake.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Juni 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Matendo ya Mitume, Filemoni na 1 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/